1 Sam 10:23-24
1 Sam 10:23-24 SUV
Basi wakaenda mbio wakamleta kutoka huko; naye aliposimama kati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wote, tangu mabega yake kwenda juu. Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na BWANA, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!