1 Yoh 4:19-21
1 Yoh 4:19-21 SUV
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.