Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 3

3
Wazawa wa Daudi na Sulemani
1 # 1 Sam 25:43; 27:3; 2 Sam 3:2; Yos 15:56 Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli; 2wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi; 3#2 Sam 3:5wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe. 4#2 Sam 2:11; 1 Fal 2:11; 2 Sam 5:5Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akamiliki miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akamiliki miaka thelathini na mitatu. 5#1 Nya 14:4; 2 Sam 12:24Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu; 6na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti; 7na Noga, na Nefegi, na Yafia; 8#2 Sam 5:14na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu kenda. 9#2 Sam 13:1; 14:27Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa umbu lao. 10#1 Fal 11:43; 14:31; 15:6Na mwanawe Sulemani alikuwa Rehoboamu; na mwanawe huyo alikuwa Abiya; na mwanawe huyo ni Asa; na mwanawe huyo ni Yehoshafati; 11na mwanawe huyo ni Yehoramu; na mwanawe huyo ni Ahazia; na mwanawe huyo ni Yoashi; 12na mwanawe huyo ni Amazia; na mwanawe huyo ni Uzia; na mwanawe huyo ni Yothamu; 13na mwanawe huyo ni Ahazi; na mwanawe huyo ni Hezekia; na mwanawe huyo ni Manase; 14na mwanawe huyo ni Amoni; na mwanawe huyo ni Yosia. 15Na wana wa Yosia walikuwa hawa; Yohana mzaliwa wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia, wa nne Shalumu. 16#Mt 1:11; 2 Fal 24:17Na wana wa Yehoyakimu ni hawa; mwanawe Yekonia, na mwanawe Sedekia. 17#Mt 1:12Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, 18na Malkiramu, na Pedaya, na Shenazari, na Yekamia, na Hoshama, na Nedabia. 19#Ezr 3:2Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa umbu lao; 20na Hashuba, na Oheli, na Berekia, na Hasadia, na Yushab-Hesedi, watu watano. 21Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.#3:21 Au, hivi, Na wana wa Hanania; Pelatia, na mwanawe huyo ni Yeshaya, na mwanawe huyo ni Refaya, na mwanawe huyo ni Arnani, na mwanawe huyo ni Obadia, na mwanawe huyo ni Shekania. 22#Ezr 8:2Na wana wa Shekania ni hawa; Shemaya, na wana wa Shemaya; Hatushi, na Igali, na Baria, na Nearia, na Shafati, watu sita. 23Na wana wa Nearia; Elioenai, na Hezekia, na Azrikamu, watu watatu. 24Na wana wa Elioenai; Hodavia, na Eliashibu, na Pelaya, na Akubu, na Yohana, na Delaya, na Anani, watu saba.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 3: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha