Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 16:23-34

1 Nya 16:23-34 SUV

Mwimbieni BWANA, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu. Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu; Tetemekeni mbele zake, nchi yote. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki; Bahari na ivume na vyote viijazavyo; Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo; Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha, Mbele za BWANA, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Soma 1 Nya 16

Picha ya aya ya 1 Nya 16:23-34

1 Nya 16:23-34 - Mwimbieni BWANA, nchi yote;
Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake.

Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;
Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
Maana miungu yote ya watu si kitu;
Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.

Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;
Leteni sadaka, mje mbele zake;
Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
Tetemekeni mbele zake, nchi yote.

Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;
Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
Bahari na ivume na vyote viijazavyo;
Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,

Mbele za BWANA,
Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;
Kwa maana fadhili zake ni za milele.