1 Nya 16:23-31
1 Nya 16:23-31 SUV
Mwimbieni BWANA, nchi yote; Tangazeni wokovu wake siku kwa siku. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake, Na watu wote habari za maajabu yake. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana; Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote. Maana miungu yote ya watu si kitu; Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu. Heshima na adhama ziko mbele zake; Nguvu na furaha zipo mahali pake. Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu, Mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake; Leteni sadaka, mje mbele zake; Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu; Tetemekeni mbele zake, nchi yote. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike; Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie; Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki