Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 6:9-15

Zekaria 6:9-15 NENO

Neno la BWANA likanijia kusema: “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku hiyo hiyo nenda nyumbani mwa Yosia mwana wa Sefania. Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uliweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki. Umwambie hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: ‘Huyu ndiye mtu anayeitwa Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu la BWANA. Ni yeye atakayejenga Hekalu la BWANA, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki kwenye kiti cha enzi. Atakuwa kuhani kwenye kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa na amani kati ya hao wawili.’ Taji litatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu la BWANA. Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu la BWANA, nanyi mtajua kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtii BWANA Mungu wenu kwa bidii.”