Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zekaria 3:1-5

Zekaria 3:1-5 NENO

Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa BWANA, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki. BWANA akamwambia Shetani, “BWANA akukemee Shetani! BWANA, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?” Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.” Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa BWANA akiwa amesimama karibu.