Zekaria 10:1-3
Zekaria 10:1-3 NENO
Mwombeni BWANA mvua wakati wa vuli; ndiye BWANA atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu. Sanamu huzungumza udanganyifu, waaguzi huona maono ya uongo; husimulia ndoto ambazo si za kweli, wanatoa faraja batili. Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo walioteseka kwa kukosa mchungaji. “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji, nami nitawaadhibu viongozi; kwa kuwa BWANA wa majeshi atalichunga kundi lake, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kama farasi mwenye kiburi akiwa vitani.