Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 91

91
Zaburi 91
Mungu mlinzi wetu
1 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,
atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.#91:1 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania.
2 Nitasema kumhusu Bwana, “Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu, ninayemtumaini.”
3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,
na maradhi ya kuambukiza ya kuua.
4 Atakufunika kwa manyoya yake,
chini ya mabawa yake utapata kimbilio,
uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.
5 Hutaogopa vitisho vya usiku,
wala mshale urukao mchana,
6wala maradhi ya kuambukiza
yanayonyemelea gizani,
wala tauni iharibuyo adhuhuri.
7Ijapo watu elfu wataangukia kando yako,
kumi elfu mkono wako wa kuume,
lakini haitakukaribia wewe.
8 Utatazama tu kwa macho yako
na kuona adhabu ya waovu.
9Ukimfanya Aliye Juu Sana kuwa makao yako;
naam, Bwana ambaye ni kimbilio langu;
10 basi hakuna madhara yatakayokupata wewe,
hakuna maafa yatalikaribia hema lako.
11 Kwa kuwa atawaagiza malaika wake kwa ajili yako,
wakulinde katika njia zako zote.
12 Watakuchukua mikononi mwao,
ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
13 Utawakanyaga simba na nyoka wakali,
simba mkubwa na nyoka utawaponda kwa miguu.
14 Bwana asema, “Kwa kuwa ananipenda, nitamwokoa;
nitamlinda, kwa kuwa analikiri Jina langu.
15 Ataniita, nami nitamjibu;
nitakuwa pamoja naye katika taabu,
nitamwokoa na kumheshimu.
16 Kwa siku nyingi nitamshibisha
na kumwonesha wokovu wangu.”

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 91: NEN

Kuonyesha

Nakili

Linganisha

Shirikisha

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia