Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 86

86
Zaburi 86
Kuomba msaada
Maombi ya Daudi.
1 Ee Bwana, sikia na unijibu,
kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.
2 Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako,
wewe ni Mungu wangu,
mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.
3 Ee Bwana, nihurumie mimi,
kwa maana ninakuita mchana kutwa.
4 Mpe mtumishi wako furaha,
kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana,
ninainua nafsi yangu.
5 Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,
umejaa upendo kwa wote wakuitao.
6 Ee Bwana, sikia maombi yangu,
sikiliza kilio changu unihurumie.
7 Katika siku ya shida yangu nitakuita,
kwa maana wewe utanijibu.
8 Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe,
hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.
9 Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya
yatakuja na kuabudu mbele zako;
wataliletea utukufu jina lako.
10 Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu;
wewe peke yako ndiwe Mungu.
11 Ee Bwana, nifundishe njia yako,
nami nitaenda katika kweli yako;
nipe moyo usiositasita,
ili niweze kulicha jina lako.
12 Ee Bwana Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote;
nitaliadhimisha jina lako milele.
13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;
umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi#86:13 Kaburi hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu..
14 Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia;
kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:
watu wasiokuheshimu wewe.
15 Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira,
bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
16 Nigeukie na unihurumie;
mpe mtumishi wako nguvu zako,
mwokoe mwana wa mjakazi wako#86:16 au mwokoe mwanao mwaminifu.
17 Nipe ishara ya wema wako,
ili adui zangu waione nao waaibishwe,
kwa kuwa wewe, Ee Bwana,
umenisaidia na kunifariji.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 86: NEN

Kuonyesha

Nakili

Linganisha

Shirikisha

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia