Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 84

84
Zaburi 84
Kuionea shauku nyumba ya Mungu
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya wana wa Kora.
1 Ee Bwana wa majeshi,
makao yako yapendeza kama nini!
2 Nafsi yangu inatamani sana,
naam, hata kuona shauku,
kwa ajili ya nyua za Bwana;
moyo wangu na mwili wangu
vinamlilia Mungu Aliye Hai.
3 Hata shomoro amejipatia makao,
mbayuwayu amejipatia kiota
mahali awezapo kuweka makinda yake:
mahali karibu na madhabahu yako,
Ee Bwana wa majeshi,
Mfalme wangu na Mungu wangu.
4Heri wale wanaokaa nyumbani mwako,
wanaokusifu wewe daima.
5 Heri wale ambao nguvu zao ziko kwako,
na njia ziendazo Sayuni zimo mioyoni mwao.
6 Wanapopita katika Bonde la Baka#84:6 maana yake Bonde la Vilio,
hulifanya mahali pa chemchemi,
pia mvua za vuli hulijaza kwa madimbwi#84:6 au baraka.
7 Huendelea toka nguvu hadi nguvu,
hadi kila mmoja afikapo
mbele za Mungu huko Sayuni.
8 Ee Bwana Mungu wa majeshi, sikia maombi yangu;
nisikilize, Ee Mungu wa Yakobo.
9 Ee Mungu, uitazame ngao yetu,
mtazame kwa wema mpakwa mafuta wako.
10 Siku moja katika nyua zako ni bora
kuliko siku elfu mahali pengine;
afadhali ningekuwa bawabu katika nyumba ya Mungu wangu
kuliko kukaa katika mahema ya waovu.
11 Kwa kuwa Bwana Mungu ni jua na ngao;
Bwana hutoa wema na heshima;
hakuna kitu chema anachowanyima
wale ambao hawana hatia.
12 Ee Bwana wa majeshi,
heri mtu anayekutumaini wewe.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 84: NEN

Kuonyesha

Nakili

Linganisha

Shirikisha

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia