Zaburi 51:1-3
Zaburi 51:1-3 NENO
Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu. Kwa maana najua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima.