Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 38:11-22

Zaburi 38:11-22 NENO

Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani wangu wanakaa mbali nami. Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea kuhusu maangamizi yangu; hupanga hila mchana kutwa. Mimi ni kama kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake; nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu. Ee BWANA, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu. Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wajitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.” Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote. Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu. Wengi wamekua adui zangu bila sababu; wale wanaonichukia bure ni wengi. Wanaolipa wema wangu kwa maovu hunisingizia ninapofuata lililo jema. Ee BWANA, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu. Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia.