Zaburi 19:7-14
Zaburi 19:7-14 NENO
Sheria ya BWANA ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za BWANA ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. Maagizo ya BWANA ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za BWANA huangaza, zatia nuru machoni. Kumcha BWANA ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za BWANA ni za hakika, nazo zina haki. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka sega. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa. Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua. Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, niwe huru na hatia kubwa. Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.