Zaburi 16:9-11
Zaburi 16:9-11 NENO
Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao utapumzika salama, kwa maana hutaniacha Kuzimu, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. Umenijulisha njia ya uzima; utanijaza na furaha mbele zako, pamoja na furaha ya milele katika mkono wako wa kuume.