Zaburi 150
150
Zaburi 150
Msifuni Bwana kwa ukuu wake
1Msifuni Bwana.#150:1 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 150:6.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
2Msifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
4msifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5msifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.
Msifuni Bwana!
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 150: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.