Zaburi 123:1-4
Zaburi 123:1-4 NENO
Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi. Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mjakazi yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo BWANA Mungu wetu, hadi atakapotuhurumia. Uturehemu, Ee BWANA, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi. Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.