Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 107:10-22

Zaburi 107:10-22 NENO

Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu, wafungwa wakiteseka katika minyororo, kwa sababu waliasi dhidi ya maneno ya Mungu, na kudharau ushauri wa Aliye Juu Sana. Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwa na mtu wa kuwasaidia. Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. Akawatoa katika giza na huzuni kuu na akavunja minyororo yao. Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu, kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba na kukata mapingo ya chuma. Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao, wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao. Wakachukia kabisa vyakula vyote, wakakaribia malango ya mauti. Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizi yao. Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.