Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 3:27-35

Mithali 3:27-35 NENO

Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. Usipange mabaya dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe kwa uaminifu. Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakudhuru kwa lolote. Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake yoyote, kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. Laana ya BWANA i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu na walioonewa. Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.