Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 14:5-14

Mithali 14:5-14 NENO

Shahidi mwaminifu hadanganyi, bali shahidi wa uongo humimina uongo. Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati, bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua. Kaa mbali na mtu mpumbavu, kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake. Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake, bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu. Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi, bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu. Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe, wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake. Nyumba ya mwovu itaangamizwa, bali hema la mnyofu litastawi. Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. Hata katika kicheko moyo unaweza kuuma, nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi. Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao, naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.