Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wafilipi 1:1-6

Wafilipi 1:1-6 NENO

Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu. Kwa watakatifu wote katika Kristo Yesu walio Filipi, pamoja na maaskofu na mashemasi. Neema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo ziwe nanyi. Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi. Katika maombi yangu yote daima nimekuwa nikiwaombea ninyi nyote kwa furaha, kwa sababu ya kushiriki kwenu katika kueneza Injili, tangu siku ya kwanza hadi leo. Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu.