Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko Utangulizi

Utangulizi
Yohana Marko, mwandishi wa Injili hii, alitajwa na mababa wa kanisa la mwanzo, yaani Papiasi, Irenio na Klementi wa Iskanderia, kuwa mshirika wa karibu sana wa Mtume Petro. Yohana Marko alikuwa mtoto wa Maria, ambaye nyumba yake ilikuwa kituo kikuu cha Ukristo huko Yerusalemu. Hatimaye Marko aliishi Rumi ambako aliandika kumbukumbu za Mtume Petro.
Marko alisafiri na mjomba wake, Barnaba, kwenda Antiokia ya Syria walipofuatana na Paulo kwenye safari yake ya kwanza ya kitume. Hata hivyo Marko aliwaacha Barnaba na Paulo huko Kipro na kurudi Yerusalemu. Baadaye Barnaba na Marko walielekea Kipro wakati Paulo alienda Asia. Miaka kama kumi baadaye, Marko alikuwa pamoja na Paulo huko Rumi. Shabaha ya Marko ilikuwa kukusanya pamoja ujumbe wote wa Injili kwa kifupi.
Mwandishi
Yohana Marko.
Kusudi
Kumtambulisha Yesu, kazi, na mafundisho yake.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Kati ya 55–65 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu Kristo na wanafunzi wake, Pilato, na viongozi wa dini ya Kiyahudi.
Wazo Kuu
Marko anamdhihirisha Bwana Yesu kuwa Mtumishi wa Mungu, na Mtu wa vitendo aliyekuja kuyatimiza mapenzi ya Mungu.
Mambo Muhimu
Marko anaanza kwa kueleza habari za huduma ya Bwana Yesu hadharani na mahubiri yake kuhusu Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Kisha anatoa wazi unabii kuhusu matazamio ya kifo cha Bwana Yesu. Hatimaye anaeleza jinsi Bwana Yesu alivyosulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na alivyofufuliwa kutoka kwa wafu; pia maneno na maagizo yake ya mwisho kwa wanafunzi wake.
Mgawanyo
Yohana Mbatizaji, na ubatizo wa Bwana Yesu (1:1-13)
Huduma ya Yesu huko Galilaya (1:14–9:50)
Safari ya kwenda Yerusalemu na kuingia mjini (10:1–11:26)
Matatizo mjini Yerusalemu (11:27–12:44)
Unabii kuhusu mambo yajayo (13:1-37)
Kufa na kufufuka kwa Yesu (14:1–16:20).

Iliyochaguliwa sasa

Marko Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha