Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Marko 15:40-47

Marko 15:40-47 NENO

Palikuwa na wanawake waliokuwa wakiangalia kwa mbali. Miongoni mwao walikuwa Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, pia na Salome. Hawa walifuatana na Yesu na kushughulikia mahitaji yake alipokuwa Galilaya. Pia walikuwako wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja pamoja naye hadi Yerusalemu. Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa Siku ya Maandalizi (yaani siku moja kabla ya Sabato), Yusufu wa Arimathaya, mtu aliyeheshimiwa katika Baraza, na alikuwa anautarajia ufalme wa Mungu, akamwendea Pilato kwa ujasiri na kumwomba mwili wa Yesu. Pilato alikuwa akijiuliza kama Yesu alikuwa amekwisha kufa. Hivyo akamwita yule jemadari, akamuuliza iwapo Yesu alikuwa amekwisha kufa. Baada ya kupata habari kutoka kwa yule jemadari kwamba kweli amekwisha kufa, Pilato akampa Yusufu ruhusa ya kuuchukua huo mwili. Hivyo Yusufu akanunua kitambaa cha kitani safi, akaushusha mwili kutoka msalabani, akaufunga katika kile kitambaa cha kitani, na kuuweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kwenye ingilio la kaburi. Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose walipaona mahali pale alipolazwa.