Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 4:1-11

Mathayo 4:1-11 NENO

Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu hadi nyikani ili ajaribiwe na ibilisi. Baada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. Mjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.” Lakini Yesu akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’” Ndipo ibilisi akampeleka Yesu hadi mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, akamwambia, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika wake, nao watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’” Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’” Kwa mara nyingine, ibilisi akampeleka Yesu hadi kwenye kilele cha mlima mrefu na kumwonesha falme zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote ukinisujudia na kuniabudu.” Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’” Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.