Mathayo 22:1-3
Mathayo 22:1-3 NENO
Yesu akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. Akawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.