Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 16:5-8

Luka 16:5-8 NENO

“Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa bwana wake, mmoja mmoja. Akamuuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo mia moja vya mafuta ya mizeituni.’ “Msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati ya deni lako, ibadilishe upesi, uandike vipimo hamsini.’ “Kisha akamuuliza wa pili, ‘Wewe deni lako ni kiasi gani?’ “Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ “Yule msimamizi akamwambia, ‘Chukua hati yako, uandike vipimo mia nane!’ “Yule bwana akamsifu yule msimamizi dhalimu kwa jinsi alivyotumia ujanja. Kwa maana watu wa dunia hii wana ujanja zaidi wanapojishughulisha na mambo ya dunia kuliko watu wa nuru.