Luka 16:1-2
Luka 16:1-2 NENO
Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na msimamizi wake. Huyo msimamizi alishitakiwa kwake kwamba alikuwa akitapanya mali ya tajiri yake. Hivyo huyo tajiri akamwita na kumuuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayoyasikia kukuhusu? Toa taarifa ya usimamizi wako, kwa sababu huwezi kuendelea kuwa msimamizi.’