Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 11:1-4

Luka 11:1-4 NENO

Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.” Akawaambia, “Mnapoomba, semeni: “ ‘Baba yetu [uliye mbinguni], jina lako litukuzwe, [ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.] Utupatie kila siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni [bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu].’ ”