Walawi 2:1-3
Walawi 2:1-3 NENO
“ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa BWANA, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake, naye atapeleka kwa makuhani wana wa Haruni. Kuhani atachukua konzi moja unga laini na mafuta, pamoja na uvumba wote, na kuviteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza BWANA. Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Haruni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwa BWANA kwa moto.