Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maombolezo 2:1-6

Maombolezo 2:1-6 NENO

Tazama jinsi Bwana alivyomfunika Binti Sayuni kwa wingu la hasira yake! Ameitupa chini fahari ya Israeli kutoka mbinguni hadi duniani, hakukumbuka kiti chake cha kuwekea miguu katika siku ya hasira yake. Bila huruma Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo; katika ghadhabu yake amebomoa ngome za Binti Yuda. Ameuangusha ufalme wake na wakuu wake chini kwa aibu. Katika hasira kali amevunja kila pembe ya Israeli. Ameuondoa mkono wake wa kuume alipokaribia adui. Amemteketeza Yakobo kama moto uwakao ule uteketezao kila kitu kinachouzunguka. Ameupinda upinde wake kama adui, mkono wake wa kuume uko tayari. Kama vile adui amewaua wote waliokuwa wanapendeza jicho, amemwaga ghadhabu yake kama moto juu ya hema la Binti Sayuni. Bwana ni kama adui; amemmeza Israeli. Ameyameza majumba yake yote ya kifalme na kuangamiza ngome zake. Ameongeza huzuni na maombolezo kwa Binti Yuda. Ameharibu maskani yake kama bustani, ameharibu mahali pake pa mkutano. BWANA amemfanya Sayuni kusahau sikukuu zake zilizoamriwa na Sabato zake; katika hasira yake kali amewadharau mfalme na kuhani.