Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yona 4:1-5

Yona 4:1-5 NENO

Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika. Akamwomba BWANA, “Ee BWANA, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharakisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa. Sasa, Ee BWANA, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.” Lakini BWANA akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?” Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.