Ayubu 36:26-33
Ayubu 36:26-33 NENO
Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki. “Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka vijito; mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu. Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka kwenye hema lake. Tazama anavyotandaza radi yake kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari. Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi. Huujaza mkono wake kwa radi, na kuiagiza kulenga shabaha yake. Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.