Yakobo Utangulizi
Utangulizi
Waraka wa Yakobo unaweza kuwa mojawapo ya nyaraka za kwanza kabisa katika Agano Jipya. Inawezekana uliandikwa wakati moja na ule wa Paulo kwa Wagalatia. Waraka huu uliandikiwa Wakristo wa Kiyahudi waliotawanyika huko Ponto, Galatia, Kapadokia, jimbo la Asia, na Bithinia ili kuwapa mawaidha kuhusu ilivyowapasa kuishi kama waumini, wakidhihirishwa na matendo mema na imani itendayo kazi. Barua hii ina mithali nyingi fupi fupi zinazosaidia kuweka wazi yale Mafundisho ya Mlimani ya Bwana Yesu.
Matatizo yanayozungumziwa yalikuwa yakiwasumbua waumini. Tunasoma kuhusu kiburi, ubaguzi, choyo, tamaa, unafiki, kupenda anasa, na kusengenya. Yakobo aliandika kusahihisha makosa haya kwa kuonesha kwamba imani pasipo matendo imekufa. Hii ina maana kuwa, kusema tu kwamba unaamini hakutoshi, bali imani halisi huambatana na matendo.
Mwandishi
Yakobo, ndugu yake Yesu.
Kusudi
Kuwahimiza waumini kufanya mabadiliko yanayohitajika katika maisha ya Mkristo.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 49 B.K.
Wahusika Wakuu
Yakobo, na Wayahudi waliotawanyika sehemu mbalimbali.
Wazo Kuu
Yakobo anasisitiza umuhimu wa Mkristo kuishi maisha yanayodhihirisha hali yake ya ndani. Hapo ndipo ulimwengu utapata kujua jinsi Injili inavyoweza kubadili maisha ya watu.
Mambo Muhimu
Imani pasipo matendo imekufa; ili kuitimiza sheria ya upendo lazima imani yetu iwe na matendo. Yakobo anawafundisha Wakristo kutokubaliana na hali ya kidunia kuhusu mali na utajiri. Wakristo wanatakiwa kujiwekea hazina kwa Mungu; hivyo Wakristo hawapaswi kuwapendelea wenye mali, wala kuwadharau maskini. Pia waombe hekima kutoka kwa Mungu.
Yaliyomo
Salamu, na maisha ya imani ya kweli (1:1‑27)
Upendeleo, imani ya kweli na matendo (2:1‑26)
Kuutawala ulimi (3:1‑18)
Mwenendo upasao (4:1‑17)
Mawaidha ya mwisho (5:1‑20).
Iliyochaguliwa sasa
Yakobo Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.