Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 4:12-19

Hosea 4:12-19 NENO

wa watu wangu. Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti nao hujibiwa na fimbo ya mti. Roho ya ukahaba imewapotosha, hawana uaminifu kwa Mungu wao. Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima, chini ya mialoni, milibua na miela, ambako kuna vivuli vizuri. Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba na wake za wana wenu uzinzi. “Sitawaadhibu binti zenu wakati wanapogeukia ukahaba, wala wake za wana wenu wanapofanya uzinzi, kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya na kutambikia pamoja na makahaba wa mahali pa ibada za sanamu: watu wasiokuwa na ufahamu wataangamia! “Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli, Yuda naye asije akawa na hatia. “Usiende Gilgali, usipande kwenda Beth-Aveni. Wala usiape, ‘Hakika kama BWANA aishivyo!’ Waisraeli ni wakaidi, kama ndama jike mkaidi. Ni jinsi gani basi BWANA anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani? Efraimu amejiunga na sanamu, achana naye! Hata wakati wamemaliza vileo vyao wanaendelea na ukahaba wao, watawala wao hupenda sana njia za aibu. Kisulisuli kitawafagilia mbali na dhabihu zao zitawaletea aibu.