Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hosea 4:1-11

Hosea 4:1-11 NENO

Sikieni neno la BWANA, enyi Waisraeli, kwa sababu BWANA analo shtaka dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi: “Hakuna uaminifu, hakuna upendo, hakuna kumjua Mungu katika nchi. Kuna kulaani tu, uongo na uuaji, wizi na uzinzi, bila kuwa na mipaka, nao umwagaji damu mmoja baada ya mwingine. Kwa sababu hii nchi huomboleza, wote wanaoishi ndani yake wanadhoofika; wanyama wa kondeni, ndege wa angani na samaki wa baharini wanakufa. “Lakini mtu yeyote na asilete shtaka, mtu yeyote na asimlaumu mwenzake, kwa maana watu wako ni kama wale waletao mashtaka dhidi ya kuhani. Unajikwaa usiku na mchana, nao manabii hujikwaa pamoja nawe. Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako: watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. “Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako mimi nami sitawajali watoto wako. Kadiri makuhani walivyoongezeka, ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu, walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu. Wanajilisha dhambi za watu wangu na kupendezwa na uovu wao. Hata itakuwa: Kama walivyo watu, ndivyo walivyo makuhani. Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao na kuwalipa kwa matendo yao. “Watakula lakini hawatashiba; watajiingiza katika ukahaba lakini hawataongezeka, kwa sababu wamemwacha BWANA na kujiingiza wenyewe katika ukahaba; kunywa divai ya zamani na divai mpya huondoa ufahamu