Mwanzo 27:41-46
Mwanzo 27:41-46 NENO
Esau akawa na kinyongo dhidi ya Yakobo kwa ajili ya baraka ambazo baba yake alikuwa amembariki. Akasema moyoni mwake, “Siku za kuomboleza kwa ajili ya baba yangu zimekaribia; ndipo nitamuua ndugu yangu Yakobo.” Rebeka alipoambiwa yale Esau mwanawe mkubwa aliyoyasema, akamtumania Yakobo mwanawe mdogo, akamwambia, “Ndugu yako Esau anajifariji kwa wazo la kukuua. Sasa basi, mwanangu, fanya nisemalo: Kimbilia haraka kwa Labani ndugu yangu kule Harani. Ukae naye kwa muda hadi ghadhabu ya ndugu yako itulie. Ndugu yako atakapokuwa hana hasira nawe tena na amesahau uliyomtendea, nitakupelekea ujumbe urudi. Kwa nini niwapoteze nyote wawili siku moja?” Kisha Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechukia maisha kwa sababu ya hawa wanawake Wahiti. Ikiwa Yakobo ataoa mke miongoni mwa wanawake wa nchi hii, wanawake Wahiti kama hawa, sitaona haja ya kuendelea kuishi.”