Mwanzo 25:19-23
Mwanzo 25:19-23 NENO
Hivi ndivyo vizazi vya Isaka mwana wa Abrahamu. Abrahamu akamzaa Isaka. Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu. Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. BWANA akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. Watoto wakashindana tumboni mwake, naye akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza BWANA. BWANA akamjibu, “Mataifa mawili yamo tumboni mwako, na mataifa hayo mawili kutoka ndani yako watatenganishwa. Mmoja atakuwa na nguvu kuliko mwingine, na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”


