Ezekieli 2
2
Wito wa Ezekieli
1 Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami.
3 Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, taifa ambalo limeniasi mimi; wao na baba zao wameniasi hadi leo. 4Watu ninaokutuma kwao ni wakaidi na wabishi. Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi.’ 5Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya uasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. 6Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao. Usiogope, ijapo michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ijapo wao ni nyumba ya uasi. 7Lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni waasi. 8Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiasi kama hiyo nyumba ya uasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.”
9 Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na kitabu, 10ambacho alikikunjua mbele yangu. Pande zote mbili kilikuwa kimeandikwa maneno ya maombolezo, na vilio na ole.
Iliyochaguliwa sasa
Ezekieli 2: NEN
Kuonyesha
Nakili
Linganisha
Shirikisha
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Holy Bible, Kiswahili Contemporary Version™ (Neno: Biblia Takatifu™) | Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.
Biblica® Cross Reference System | Copyright © 2025 by Biblica, Inc. | Used with permission. All rights reserved worldwide.