Waefeso 6:21-24
Waefeso 6:21-24 NENO
Tikiko, aliye ndugu mpendwa na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawaambia kila kitu, ili pia mpate kujua hali yangu na kile ninachofanya. Ninamtuma kwenu kwa ajili ya kusudi hili hasa, ili mpate kujua hali yetu, na awatie moyo. Amani iwe kwa ndugu, na pendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo. Neema iwe na wote wanaompenda Bwana wetu Yesu Kristo kwa upendo wa dhati. Amen.


