Wakolosai 3:18-21
Wakolosai 3:18-21 NENO
Ninyi wake, watiini waume zenu, kama inavyostahili katika Bwana. Ninyi waume, wapendeni wake zenu, wala msiwe wakali kwao. Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii inampendeza Bwana. Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.