Matendo Utangulizi
Utangulizi
Kitabu hiki ni cha pili katika vitabu viwili ambavyo Luka alimwandikia Theofilo. Kinajihusisha na huduma ya wafuasi wa Kristo. Luka anaonesha hali ambayo Kanisa la kwanza lilikabiliwa nayo wakati wa kuenea kwake katika utawala wa Rumi. Anathibitisha kuwa kazi ambayo Yesu alianzisha alipokuwa duniani, aliendelea kuifanya katika kanisa lake kupitia kwa Roho Mtakatifu. Katika kuenea kwa Ukristo, mkazo mkubwa uliwekwa kwa mitume kuwezeshwa na Roho Mtakatifu.
Petro ndiye anayeonekana sana wakati wa kuanzishwa kwa kanisa huko Yerusalemu. Tunaona jinsi kituo cha Ukristo kilihama hadi Antiokia ya Siria. Luka pia alionesha vile Paulo, ambaye alikuwa mtesi wa kanisa, hatimaye aliokoka na akawa kiongozi mkuu wa kanisa. Hivyo sehemu ya mwisho ya kitabu hiki imetoa nafasi kubwa kwa Paulo na utume wake. Kitabu kinaishia Paulo akiwa mfungwa anayehubiri Habari Njema huko Rumi.
Mwandishi
Luka.
Kusudi
Kueleza utendaji wa Roho Mtakatifu na wa mitume katika kulithibitisha Neno la Mungu, na pia kutoa maelezo kuhusu kuanza kwa Ukristo, na jinsi Mungu alivyodhihirisha nafsi yake mwenyewe katika mwili wa Yesu Kristo kupitia kwa kanisa.
Mahali
Hapajulikani.
Tarehe
Mnamo 63–70 B.K.
Wahusika Wakuu
Petro, Paulo, Stefano, Filipo na Barnaba.
Wazo Kuu
Kueleza jinsi Injili ilivyoenezwa kutoka kwa Wayahudi na kuwafikia watu wa mataifa mengine, na vile Injili ya kufa na kufufuka kwake Yesu ilivyo kiini cha msingi wa imani ya Ukristo.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinatoa kumbukumbu ya kuenea kwa Ukristo, kushuka kwa Roho Mtakatifu katika kanisa ili kuwatia mitume nguvu ya kuendeleza kazi ya Kristo. Kinaelezea jinsi Habari Njema ya Kristo ilivyoenea katika utawala wa Rumi, kuanzia Yerusalemu hadi Rumi.
Yaliyomo
Kanisa la kwanza (1:1–5:42)
Mateso na kuenea kwa Injili (6:1–9:31)
Matendo ya Petro (9:32–12:25)
Safari ya kwanza ya Paulo kueneza Injili (13:1–14:28)
Baraza la Yerusalemu na matokeo yake (15:1‑35)
Safari ya pili ya Paulo kueneza Injili (15:36–18:22)
Safari ya tatu ya Paulo kueneza Injili (18:23–21:16)
Kukamatwa kwa Paulo na safari yake kwenda Rumi (21:17–28:31).
Iliyochaguliwa sasa
Matendo Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.