Matendo 18:2-3
Matendo 18:2-3 NEN
Huko akakutana na Myahudi mmoja jina lake Akila, mzawa wa Ponto, aliyekuwa amewasili karibuni kutoka Italia pamoja na mkewe Prisila, kwa sababu Klaudio alikuwa ameamuru Wayahudi wote waondoke Rumi. Paulo akaenda kuwaona, naye kwa kuwa alikuwa mtengeneza mahema kama wao, akakaa na kufanya kazi pamoja nao.



