1 Timotheo 1:1-7
1 Timotheo 1:1-7 NENO
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu, na ya Kristo Yesu aliye tumaini letu. Kwa Timotheo, mwanangu halisi katika imani. Neema, rehema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Kama nilivyokusihi wakati nilipoenda Makedonia, endelea kubaki Efeso, ili upate kuwaagiza watu wasiendelee kufundisha mafundisho ya uongo wala wasitoe muda wao kwa hadithi za kubuniwa na orodha za majina ya vizazi visivyo na mwisho, ambazo huchochea mabishano badala ya mpango wa Mungu utokanao na imani. Kusudi la maagizo haya ni upendo unaotoka katika moyo safi, dhamiri safi na imani ya kweli. Watu wengine wamepotoka kutoka haya na kugeukia majadiliano yasiyo na maana kwa kuwa, wanataka kuwa walimu wa sheria, lakini hawajui mambo yale wanayosema wala hayo wanayoyatumainia kwa uthabiti.


