1 Wafalme 19:11-14
1 Wafalme 19:11-14 NENO
BWANA akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za BWANA, kwa kuwa BWANA yu karibu kupita hapo.” Kisha upepo mzito na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za BWANA, lakini BWANA hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la ardhi, lakini BWANA hakuwamo kwenye lile tetemeko. Baada ya tetemeko la ardhi moto ukaja, lakini BWANA hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona. Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mlango wa pango. Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?” Akajibu, “Nimekuwa nikifanya bidii sana kwa ajili ya BWANA Mungu wa majeshi. Waisraeli wamelikataa agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi peke yangu niliyebaki, sasa wananitafuta ili waniue pia.”


