Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohana Utangulizi

Utangulizi
Wasomi wa waraka huu walikumbwa na mafundisho hatari sana ya Wanostiki, waliofundisha kuwa kila kitu kilikuwa kiovu, isipokuwa roho pekee ndiyo nzuri. Kati ya mafundisho yao, walikana imani za msingi za Kikristo kama: hali ya Kristo kuja katika mwili, mamlaka ya amri ya Kristo, hali ya mwanadamu kuwa mwenye dhambi, na wokovu kuwa ni kazi ya Kristo.
Mwandishi wa waraka huu aligundua ya kuwa jamii ya waumini ilikuwa katika hatari kubwa. Anawakumbusha waumini kuhusu umuhimu wa kuihifadhi imani, na kuwaeleza kuwa Kristo alikuja katika mwili.
Mwandishi
Mtume Yohana.
Kusudi
Yohana anaonyesha wazi kuwa Yesu ni Mungu aliyefanyika mwili, na hivyo kupinga kabisa ile dhana kwamba Kristo aliwaziwa tu kama aliyekuwa na mwili, eti kwamba yeye alikuwa roho.
Mahali
Efeso.
Tarehe
Kati ya 85–90 B.K.
Wahusika Wakuu
Yohana na Yesu.
Wazo Kuu
Si jambo gumu kupingana na mafundisho yanayokataa wazi misingi ya imani. Lakini mawazo potovu yanayofanana na kweli ya Injili yanapoingia, basi hili linakuwa tatizo kubwa.
Mambo Muhimu
Mwana wa Mungu alikuja ulimwenguni katika mwili, alisikika na watu, alionekana, aligusika na walimkazia macho. Waraka huu unatangaza imani ya kweli katika Kristo ni imani katika Mungu kufanyika mwili, na maisha ya Kikristo ni upendano wa ndugu.
Mgawanyo
Utangulizi (1:1-4)
Umuhimu wa nuru katika ushirika (1:5–2:29)
Upendo sharti uenee katika maisha (3:1–4:21)
Imani na kuona kwa hakika (5:1-21).

Iliyochaguliwa sasa

1 Yohana Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha