Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 4:14-21

1 Wakorintho 4:14-21 NENO

Siwaandikii mambo haya ili kuwaaibisha, bali ili kuwaonya, kama wanangu wapendwa. Hata kama mnao walimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili. Basi nawasihi igeni mfano wangu. Kwa sababu hii ninamtuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu njia za maisha yangu katika Kristo Yesu, ambayo yanakubaliana na mafundisho yangu ninayofundisha katika kila kanisa. Baadhi yenu mmekuwa na jeuri mkidhani kuwa sitafika kwenu. Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu hivi karibuni, nami nitajua, si tu kile wanachosema hawa watu jeuri, bali pia nguvu yao. Kwa kuwa ufalme wa Mungu si maneno matupu tu bali ni nguvu. Ninyi amueni. Je, nije kwenu na fimbo, au nije kwa upendo na kwa roho ya upole?