Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 16:13-24

1 Wakorintho 16:13-24 NENO

Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari. Fanyeni kila kitu katika upendo. Ninyi mnajua kwamba watu wa nyumbani mwa Stefana ndio walikuwa wa kwanza kuamini katika Akaya, nao wamejitoa kwa ajili ya kuwahudumia watakatifu. Ndugu nawasihi, mjitie katika kuwahudumia watu kama hawa na kila mmoja aingiaye kwenye kazi na kuifanya kwa bidii. Nilifurahi Stefana, Fortunato na Akaiko walipofika, kwa sababu wamenipatia yale niliyopungukiwa kutoka kwenu. Kwa kuwa waliiburudisha roho yangu na zenu pia. Watu kama hawa wanastahili kutambuliwa. Makanisa ya jimbo la Asia yanawasalimu. Akila na Prisila pamoja na kanisa lililoko nyumbani mwao wanawasalimu sana katika Bwana. Ndugu wote walio hapa wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu. Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kama mtu yeyote hampendi Bwana Yesu Kristo, na alaaniwe. Bwana wetu, njoo. Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi. Upendo wangu uwe nanyi nyote katika Kristo Yesu. Amen.