Ndipo, nitakapoyatowesha magari kule Efuraimu,
nao farasi mle Yerusalemu,
nazo pindi za vita zitatoweshwa,
nao wamizimu atawafundisha kutengemana;
ufalme wake utaanzia baharini, uifikie bahari ya pili,
tena uanzie penye jito kubwa, uyafikie mapeo ya nchi.