Haya ndiyo maagizo, mtakayoyafanya: Semeni yaliyo kweli kila mtu na mwenziwe, tena kateni malangoni kwenu mashauri yaliyo sawa! Mtu na mwenziwe msiwaziane mabaya mioyoni mwenu, wala msipende kuapa viapo vya uwongo! Kwani hayo yote ndiyo, ninayochukizwa nayo; ndivyo, asemavyo Bwana.