Alipokwisha kukaa kwao siku zisizopita nane au kumi, akatelemka kwenda Kesaria. Kesho yake akaketi katika kiti cha uamuzi, akaagiza, Paulo aletwe. Alipofika, Wayuda waliotelemka toka Yerusalemu wakamsimamia pande zote, wakamsingizia mambo mengi yaliyokuwa magumu, wasiweze kuyaonyesha kuwa ya kweli.